Wajanja Tumewahi Official Video - Neema Mwaipopo 2015
Mwanadada Muimbaji wa nyimbo za Injili hapa Tanzania Neema Mwaipopo anatoleo jipya albam yake mpya inayokwenda kwa jina la WAJANJA TUMEWAHI.
albam yake mpya ambapo ametanabaisha kuwa ni albam ambayo ni nzuri na kudai kuwa wadau wa nyimbo za injili wataipenda zaidi.
albam hii mpya itakuwa na nyimbo 11 ikiongozwa na wimbo uliobeba albam unaoitwa Wajanja tumewahi.
Neema aliamua kuweka nyimbo nyingi ili kuwapa fulsa wasikilizaji kujichagulia nyimbo za kusikiliza.
Hii ni albam ya tatu ya Neema kwani hapo awali alitamba na albam iliyokwenda kwa jina la Usijinyime raha baadaye akatamba na wimbo wa Jifunze kunyamaza, hivi sasa anakuja na Wajanja Tumewahi.
Neema amewaomba wadau wa nyimbo za injili kusikiliza hii albam kwani alisema kuwa ni nzuri na Mungu ameipaka mafuta kwa injili.