Thamani ya Wokovu Wangu - Christina Shusho
[download id=”4330″]
Ngoja nikusimulie, habari ya kijana mmoja,
Kijana mtanashati, mpole kipenzi cha wengi,
Anazo sifa nyingi lakini kuu kwake ni upendo,
Siku moja alikutana na mwanamke msamaria kisimani
Kijana kamwomba maji, mwanamke naye kamuuliza,
Tangu lini wayahudi na wasamaria tukashikamana
Kijana akamwambia ungejua mimi ni maji yaliyo hai,
Ungekuja kwangu unywe maji, ili usiwe na kiu tena.
Mimi aliniona nilikokuwa nimechoka, nimechakaa,
Kijana kanipenda, kanichukua kanitengenezaaa
Chorus
Thamani ya Wokovu wangu anayejua ni Mwokozi wangu,
Gharama ya maisha yangu anayejua ni Muumba,
Nikisema nimeokokaa mbona hamnielewiii,
Nikisema nimependwa mie, mbona mwanishangaaa
Maisha ni hazina, iliyo mikononi mwa Mungu
Hakuna ajuaye, salio la siku zake
Ukiona ni mzima leo, hujui kesho itakuwaje?
Ndiyo maana nimeona nikukumbushe habari za Yesu
Yeye akikupenda, wala hatoitoi kasoro
Ukimupokea leo anabadili historia yako
Atakuchukua hivyo ulivyo akufanye kiumbe kipya
Hata kama unalia leo jua kesho utacheka
Huyu Mwanaume Yesu ni wa ajabu wala hana mfano wake
Upendo wake ulivyo mkuu kwetu akajiona heri ajitoe
Aliacha enzi na utukufu mbinguni,
Akakubali mateso hata kifo cha aibu,
Akavuliwa nguo, ili mimi nipone,
Akatemewa mate ili mimi niwe huru
Chorus
Thamani ya Wokovu wangu anayejua ni Mwokozi wangu,
Gharama ya maisha yangu anayejua ni Muumba,
Nikisema nimeokokaa mbona hamnielewiii,
Nikisema nimependwa mie, mbona mwanishangaaa