Ni Tabibu wa Karibu na Angela Chibalonza
Ni Tabibu wa Karibu ni wimbo kutoka katika kitabu cha tenzi za rohoni #7 lakini pia unapatikana katika vitabu vingine vya kikristo. Wimbo huu una mvuto na upako wa kipekee hasa katika maeneo ya kumsifu, kumuabudu, kumtukuza, kumnyenyekea, kutubu, kumpenda na kumtumikia Mungu wetu. Huu wimbo umeshawahi kuimbwa na waimbaji mbalimbali maarufu, kwaya na bendi maarufu.
Mwimbaji mmojawapo aliyeuimba vizuri na katika upako wa kipekee wimbo huu wa Tabibu wa Karibu ni marehemu Angela Chibalonza.
Tafadhali fuatilia wimbo wa Tabibu wa Karibu na Tuimbe Pamoja:
NI Tabibu wa Karibu, Tabibu wa ajabu
Na rehema za daima; Ni dawa yake njema
- Imbeni, malaika,
- Sifa za YESU Bwana,
- Pweke limetukuka,
- Jina Lake YESU.
Hatufai kuwa hai; Wala hatutumai
Ila yeye kweli ndiye; Atupumzishaye.
Kibwagizo
Dhambi pia na hatia;Ametuchukulia,
Twenendeni na amani; Hata kwake Mbinguni.
Kibwagizo
Huliona tamu jina,Jina Lake YESU.
Yuna sifa mwenye kufa, Asishindwe na Kufa.
Kibwagizo
Kila mume asimame, Sifa zake zivume
Wanawake na washike, Kusifu jina lake.
Kibwagizo
Na vijana wote tena, Wampendao sana
Waje kwake wawe wake, Kwa utumishi wake
Kibwagizo